Triple A FM
Triple A FM
18 September 2026, 12:30 pm

“Maeneo mawili……ndio ambayo yapo katika hatari kubwa zaidi ya kumzewa na ziwa Manayara ni kama linahama na lizanzidi kuingia kwenye makazi ya watu”
Na Joel Headman
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Reuben Kwagilwa ameuelekeza uongozi wa mkoa wa Arusha na wilaya ya Monduli kuchukua tahadhari dhidi ya athari za mvua kubwa za El Niño, ikiwemo mafuriko na tishio la ziwa Manyara kumeza makazi ya watu
Miongoni mwa hatua alizoelekeza ni kusitishwa kwa shughuli za kilimo na za kibinadamu katika maeneo hatarishi pembezoni mwa ziwa hilo, pamoja na kuandaliwa kwa mipango ya kuwalinda na, inapobidi, kuwahamisha wananchi wanaoishi katika maeneo yenye hatari kubwa ya mafuriko.
Kwagilwa ametoa maagizo hayo kwenye wilayani Monduli wakati akiendelea na ziara yake katika mikoa ya Arusha na Manyara, iliyoanza Septemba 14, 2026, yenye lengo la kukagua maeneo yaliyo katika hatari ya mafuriko na kuweka mikakati ya kuzuia na kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa
Akiwa katika maeneo ya Ziwa Manyara, ameagiza shughuli zote zinazofanyika katika maeneo hatarishi pembezoni mwa mito kusitishwa mara moja, sambamba na kuandaliwa kwa mpango wa kuwalinda wananchi wanaoishi katika maeneo ya Bonde la Ufa, hususan Kata ya Mangara

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Kwagila, mkuu wa Wilaya ya Monduli mh.Gloriana Kimath ameeleza kuwa baadhi ya kata za Wilaya hiyo ikiwemo Mto wa Mbu,Majengo na Migungani zimekuwa zikikabiliwa na mafuriko ya mara kwa mara hivyo kuhitaji hatua za haraka kuwanusuru wananchi
Mmoja wa wananchi wa Monduli ameiomba serikali kuhakikisha iwapo italazimika kuwahamisha wananchi wanaoishi maeneo hayo wapatiwe maeneo mbadala ambayo ni makubwa ili kuendelea na shughuli zao za kuwaingizia kipato kama kawaida
