Triple A FM
Triple A FM
22 September 2026, 10:30 am

“Muanze pia kuwasiliana na ndugu zenu ambao wanakaa katika maeneo ya mlimani, ambao tuna uhakika kwamba hata mvua zikiwa nyingi hawawezi kufikiwa na mafuriko”
Na Joel Headman
Katika kuhakikisha jamii inajiepusha na madhara yanayoweza kuletwa na mvua za Elnino, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Muriet jijini Arusha, amefanya ziara katika maeno tofauti ya wilaya hiyo ili kutoa elimu kwa wananchi
Mkuu huyo wa polisi SSP Daudi Mwakalobo, katika ziara hiyo amewahamasisha wananchi kuchukua hatua za mapema ili kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua za El Nino.
Miongoni wa hatua hizo ni pamoja na kuweka mazingira safi kwa kusafisha mitaro iliyoziba, kusafisha njia za maji na kuondoa uchafu unaoweza kuzuia mtiririko wa maji.
Mwakalobo pia amewa rai wananchi wanaoishi maeneo ya mabondeni kutoa taarifa mapema pindi wanapobaini uwepo wa maji mengi katika maeneo yanayowazunguka Pamoja na kuhamia kwenye maeneo salama
Wakizungumza katika ziara hiyo baadhi ya wananchi katika kata ya Olasiti wamewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuwa hakuna uhakika wa kipimo cha madhara yatakayoletwa na Elnino