Triple A FM

Arusha kukabiliana na Elnino

26 September 2026, 4:01 pm

“Unajua wananchi sisi ndio tuna mzigo mkubwa wakutokuelewa, unaona kabisa huu ni mtaro au unaona kabisa hapa ni makazi ya watu ambapo hawa watu wamekaa kistaarabu lakini….”

Na Fedrick mbaruk

Wananchi mkoani arusha wameanza kuchukua tahadhari mbalimbali, ikiwemo kuhama katika maeneo hatarishi, ili kujiweka salama dhidi ya athari za mvua za El niño zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni

Wakizungumza na redio Triple a fm kwa nyakati tofauti wananchi hao wameeleza kuchukua hatua hizo baada ya elimu waliyoipata kutoka serikalini kuhusu madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo

Miongoni mwa hatua walizochukua ni pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya mafuriko na athari nyingine kama anavyoeleza bwana Emanuel Massawe

Wananchi wakitoa maoni

                   

Kwa upande wake Christopher Johnson ameeleza kuwa licha ya jitihada zinazofanywa na serikali bado wananchi wana nafasi kubwa ya kukabiliana na madhara ya elnino ikiwemo kutunza mazingira na kuyafanya safi muda wote

Wananchi wakitoa maoni

Mapema wiki hii mkuu wa mkoa wa arusha cpa Amos Makala akiongea na wananchi wa kata ya mto wa mbu mkoani arusha ameendelea kutoa elimu ya kuwataka wananchi kujiepusha na maeneo hatarishi ili kujikinga dhidi ya madhara yanayoweza kutokea

Mkuu wa mkoa wa Arusha Amos Makala