Triple A FM

Mfungwa wa nje afariki akihusishwa na mauaji ya Bodaboda

22 October 2026, 6:08 pm

Picha ya kutengenezwa inayoonyesha mualifu akijaribu kumdhuru dereva bodaboda

“na ambapo mtuhumiwa Dickson Livingstone au Ndesaa likuwa bado anaendela kutumikia kifungo cha nje”

Na Joel Headman

Watuhumiwa wawili wa matukio ya uporaji na unyang’anyi wa kutumia silaha mkoani Arusha wamefariki wakati wakipatiwa matibabu baada ya makabiliano na Jeshi la Polisi

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani Arusha SACP Justine Masejo makabiliano hayo yalitokea Jumatano tarehe 21-2026 saa 3:30 usiku wakati watuhumiwa wakijiandaa kutekeleza uhalifu

Kupitia taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Polisi inaeleza kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakijihusisha na uhalifu wa aina tofauti ikiwemo mauaji ya waendesha pikipiki

Sauti ya kamanda wa polisi mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo

Kwa mujibu wa kamanda Masejo watuhumiwa hao wamewahi kushitakiwa na kuhukumiwa kifungo kwa makosa mbali mbali ikiwemo ya uhalifu wa kutumia silaha

Sauti ya kamanda wa polisi mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo

Matukio ya uporaji na mauaji ya madereva wa boda boda mkoani Arusha yameripotiwa kutokea mara kadhaa ambapo ndugu wa marehemu wamekuwa wakiliomba jeshi la polisi kuwasaidia kubaini watuhumiwa

Miongoni mwa matukio ya uporaji na mauaji kwa dereva bodaboda ni Pamoja na hili lililotokea mwezi wa 9 mwaka huu Jeshi la Polisi limewarai wananchi kuendelea kutoa taarifa za kihalifu na uhalifu ili watuhumiwa wabainike kwa haraka na kuchukuliwa hatua za Kisheria