Triple A FM

Mkutano wa Mabunge duniani, Machinga walalamikia fursa Arusha

3 October 2026, 7:48 am

Sikufichi nilipangiwa eneo la Ulezi hapo Florida kwa ndani tunajengewa soko kweli na mama samia mimi nilienda nilikaa miezi mitatu sijawahi kuuza hata mia yaani nilifanya sasa kuondoka kule nikawa natembeza mtaani baada ya kuona hapa nitaua watoto na njaa

Na Fedrick Mbaruku

Mkutano wa Mabunge duniani, Machinga walalamikia fursa Arusha

Wakati maandalizi ya mkutano wa 153 wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) yakiendelea kufanyika jijini Arusha, baadhi ya wafanyabiashara wadogo, wameeleza kuwa pamoja na uwepo wa wageni wanaotarajiwa kutokana na mkutano huo, bado wanakabiliwa na changamoto zinazowafanya washindwe kunufaika na fursa zitakazojitokeza

Wakizungumza jana na Triple A fm kutoa maoni kuhusiana na mkutano huo unaotarajiwa kuanza Oktoba 5-9 mwaka huu, wamesema wanapitia wakati mgumu katika kufanya shughuli zao kutokana baadhi kuondolewa katika maeneo wanayofanyia biashara bila kupata maeneo mbadala yenye mazingira rafiki ya biashara

Mfanyabiashara ndogondogo jijini Arusha

Changamoto nyingine wanayokabiliana nayo ni pale wanapokamatwa na mgambo na kunyang’anywa bidhaa zao wakati wakifanya biashara kisha kutozwa kiasi kikubwa cha fedha ili kuikomboa.

Maoni ya wananchi

Licha ya Changamoto hizo, baadhi ya wananchi wanaamini kuwa mkutano wa IPU unaweza kutoa fursa mbalimbali kwa wakazi wa Arusha, kutokana na ujio wa wageni kutoka maeneo mbalimbali.

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Arusha CPA Amos Makala aliagiza kuondolewa kwa watu wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi ndaani ya jiji la Arusha ikiwa ni mkakati wa kujiandaa dhidi ya madhara ya mvua za Elnino pamoja na michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) ambayo Arusha ni miongoni mwa maeneo yatakayofanyika nchini. Kufahamu zaidi