Triple A FM

Kocha mkuu Tusker FC aapa kufa na Singida

19 October 2026, 12:26 pm

Wachezaji wa Tusker fc (Njano na nyeusi) na mchezaji wa Singida BS (Nyeupe)wakiwania mpira kwenye mchezo wao wa jana

“Wamefunga bao la aina yake, bao ambalo unaweza kusema limetoka sayari nyingine! Lakini mchezaji wao amewafundisha somo washambuliaji wangu. Hata kama nafasi ya kufunga si nzuri sana, angalau….”

Joel Headman Nairobi

Ushindi wa bao 1-0 walioupata Singida Black Stars ya Tanzania kwenye mchezo wa mkondo wa pili hatua za awali dhini ya Tusker FC ya Kenya, Sasa umegeuka vita kamili kati ya wababe hao wa soka la Afrika Mashariki

Picha linaanza wakati mchezo huo uliopigwa jana Jumapili kwenye uwanja wa Nyayo Nairobi, Kenya baada ya goli la kushangaza lililofungwa dakika ya 7 kipindi cha pili na winga Jeancy Mboma wakati huo Tusker wakiamini waliushika mchezo

Akizungumz ana Triple A fm hapa Nairobi kocha wa Tusker fc Jullien Mette licha ya kukiri kuw Singida hawakuwa na maajabu uwanjani lakini ameapa kuushangaza ulimwengu kwani anakusudia kupindua meza kibabe nchini Tanzania kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumapili Oct 25 kwenye uwanja wa Azam fc Chamazi

Kocha wa Tusker fc Jullien Mette

Kwa upande wa Singida tumempata golikipa aliyeongoza timu hio jana kuichabanga Tusker goli 1 ambaye ni Yona Amos ameeleza kufurahishwa na ushindi na kuahidi kupambana kwenye mchezo ujao ili kutinga hatua ya makundi

Golikipa wa Singida BS Yona Amos

Huku sasa ni Hussein Masanza msemaji wa Singida BS amewapa onyo kali sana Tusker kuwa kichapo walichokipata ni cha mtoto na kwamba wakae mkao wa maumivu wiki ijayo

Hussein Masanza msemaji wa Singida BS