Triple A FM
Triple A FM
24 September 2026, 11:37 am

“Tayari mpaka sasa kuna wanafunzi zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali ambao tayari wamesha…“
Na Daudi Peter
Ukisikia fursa kwa wakati basi ndio hii ambayo wadau wa michezo tayari wameanza kuchangamkia fursa kwenye Makala ya 36 ya mashindano ya AFCON 2027.
Miongoni mwao ni mwanamke wa shoka Prisca Lema aliyeamua kuvunja viunzi na vizingiti na kuja na mchezo mpya kabisa ambao kama ukipita aisee uta enjoy mwenyewe
Unaujua mchezo wa Chess wewe?
Usijali hapa tumeongea na na bi Prisca kuhusiana na huo mchezo na ametueleza kuwa ni wa aina gani
Prisca amesema mchezo wa Chess ni mchezo mzuri na nimchezo ambao unachezwa na watu wa rika zote na humfanya mchezaji kuwa imara kiakili na kufikiri kwa haraka na hii ndio sababu ya kuanzisha mchezo huu
Mchezo wa Chess ni mchezo ambao umekuwa ukichezwa na mataifa ya Jirani lakini sasa kwa wakati huu ni zamu yetu sasa kuweza kuushuhudia mchezo huu wa Chess kupitia mashindano ya AFCON 2027