Triple A FM

Makonda awapiga ‘STOP’ Mgambo Arusha

7 October 2026, 11:08 pm

Mbunge wa Arusha Mjini na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda

Na Fedrick Mbaruku

Mbunge wa Arusha Mjini na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ametoa kauli kuhusu malalamiko ya wafanyabiashara wa Soko la Kilombero jijini Arusha, wanaodai kunyanyaswa na migambo wakati wakifanya shughuli zao za biashara.

Makonda ametoa kauli hiyo leo kwenye mkutano na wananchi wakati akikagua ujenzi wa soko jipya linalojengwa jijini Arusha lenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika eneo hilo.

Mbunge wa Arusha Mjini na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda

Kauli hiyo ya Makonda inakuja siku chache baada ya wafanyabiashara hao kuzungumza na Triple A FM kwa nyakati tofauti, wakieleza malalamiko yao kuhusu namna wanavyodai kushughulikiwa na migambo katika Soko la Kilombero.

Makonda pia amesema yupo tayari kula sahani moja na migambo hao, kauli ambayo imepokelewa kwa shangwe na Wafanyabiashara hao

Wafanyabiashara wa soko la Kilombero wakitoa maoni