Triple A FM
Triple A FM
7 October 2026, 10:02 pm

Na Furahini Sella
Jeshi la Polisi nchini limewakumbusha wananchi kutobaki nyuma kwenye jukumu la ulinzi wa raia na mali zao kwani ni wajibu wa kila mmoja kwa mujibu wa Katiba ya nchi
Kauli hiyo imetolewa mapema leo na mrakibu mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, Dkt. Ezekiel Kyogo, kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kamisheni ya polisi jamii, wakati akizungumza na Triple A fm
Dkt. Kyogo amesema Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai inatoa fursa kwa mwananchi kuchukua hatua za awali dhidi ya mtu anayetekeleza uhalifu, ikiwemo kumkamata, kabla ya kumkabidhi mtuhumiwa kwa Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.
Kyogo amesisitiza kuwa wananchi na jeshi la Polisi wanapaswa kushirikiana kwa karibu ili kuendelea kudumisha amani, utulivu na usalama wa nchi