Triple A FM

Watoto wa ‘linda mume wako’ wazazi wafunguka Arusha

30 October 2026, 2:46 pm

Na Fedrick Mbaruku

Baadhi ya akina mama mkoani Arusha wamesema matumizi ya simu na mitandao ya kijamii ni miongoni mwa changamoto zinazoathiri malezi ya watoto katika jamii ya sasa

Wzazi hao wanakiri kuwa kuna kazi ya ziada ya kufanywa na wazazi licha ya kuwa na  wajibu mkubwa wa kuendelea kuwaelekeza watoto wao katika misingi ya maadili mema.

Wameeleza hayo wakati wakizungumza na Triple A Fm leo, kufuatia mjadala ulioibuka kuhusu mwenendo wa wanafunzi waliojirekodi katika video iliyozua mjadala kuhusu wanawake na waume za watu wengine

Wazazi wakitoa maoni

Wamesema kuwa tofauti na miaka ya nyuma, ambapo upatikanaji wa taarifa ulikuwa na mipaka, maendeleo ya teknolojia yamefanya watoto kukutana kwa urahisi na maudhui mbalimbali, yakiwemo yale yanayoweza kuathiri maadili yao

Wazazi wakitoa maoni