Triple A FM
Triple A FM
30 September 2026, 9:32 am

Na Fedrick Mbaruku
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba, TMDA, imetoa wito kwa wananchi kuwa makini wakati wa kununua na kutumia dawa, hususani dawa zinazopatikana kwenye vyanzo visivyo rasmi.
Hayo yameelezwa na Maafisa kutoka mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kwenye warsha iliyowaleta pamoja wahariri wa habari kutoka kanda ya Kaskazini ikijumuisha mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro iliyofanyika mkoani Manyara.
TMDA inawasisitiza wananchi kuangalia kwa umakini taarifa muhimu zilizopo kwenye kifungashio cha dawa, ikiwemo jina la dawa, tarehe ya kutengenezwa, muda wa matumizi na hali ya kifungashio, kabla ya kuitumia ili kugundua ikiwa ni bandia, zimeharibika au zimepitwa na muda wa matumizi.
Kufuatia warsha hiyo wafamasia mkoani Arusha wamesema mwananchi anapaswa kufahamu dawa anayopewa na kuhakikisha ni dawa sahihi kwa tatizo alilonalo, huku wakitakiwa pia kuangalia muda wa matumizi wa dawa kabla ya kuanza kuitumia.
Kwa upande wa wananchi wamesisitiza umuhimu wa wataalamu wa afya kuwapatia elimu zaidi wananchi juu yamatumizi sahihi ya dawa na namna kuzingatia dozi kamili aliyopangiwa