Triple A FM
Triple A FM
9 October 2026, 7:17 am

Na Furahini Sella
Madereva wa bajaji, Hiace na bodaboda jijini Arusha wamelalamikia kupanda kwa bei ya mafuta, wakisema hali hiyo imeongeza gharama za uendeshaji na kuwaweka katika wakati mgumu huku wakishindwa kuongeza nauli kwa kiwango kinachoendana na ongezeko la gharama za mafuta kutokana na uwezo mdogo wa kiuchumi wa baadhi ya abiria.
Madereva hao wametoa malalamiko hayo leo wakati wakizungumza na Triple A FM ambapo wamesema pamoja na mafuta kupanda, gharama nyingine za uendeshaji zimeongezeka hivyo kuiomba Serikali kuwaangalia kwa kuweka mazingira yatakayowawezesha kukabiliana na ongezeko hilo bila kuathiri kipato chao
Mmoja wa madereva wa bajaji Mlemba Mwidini amesema kupanda kwa bei ya mafuta kumewaathiri madereva na abiria kwa ujumla, huku wakikabiliwa na changamoto ya kupanga nauli
Kwa upande wake, Musa Njuga, Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Daladala Arusha, amesema matarajio ya madereva yalikuwa kuona bei ya mafuta ikiendelea kushuka mwezi hadi mwezi ili kupunguza nauli ya usafirishaji