EDO Ifakara Yahamasisha Kilimo cha Mbogamboga kwa Njia Mbadala
EDO Ifakara Yahamasisha Kilimo cha Mbogamboga kwa Njia Mbadala
2 April 2026, 14:38
Picha ya Mbogamboga zinazozalishwa kwa kutumia njia mbadala na Shirika la Edo Ifakara(Picha na Kuruthum Mkata)
“Ni wakati sasa kwa wananchi kubadili mtazamo na kuanza kutumia mbinu za kisasa zaidi za kilimo,kwa kutumia njia badala ya kutegemea ardhi pekee, wananchi wanaweza kulima kwa kutumia mifuko na ndoo, maarufu kama “plastic gardening”-Mkurugenzi wa Taasisi ya EDO, Bi. Josephine Said
Na Kuruthum Mkata
Shirika lisilo kuwa la kiserikali la Enlighten Development Organization (EDO) Ifakara limeendesha kampeni ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kupanda mbogamboga kwa kutumia mifuko na ndoo, kama njia mbadala ya kilimo cha kawaida cha kutumia ardhi.
Akizungumza katika hafla ya kuhamasisha Kampeni ya umuhimu wa kupanda mboga mboga kwa kutumia njia mbadala iliyofanyika Aprili 1, 2026, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Bi. Josephine Said, amesema ni wakati sasa kwa wananchi kubadili mtazamo na kuanza kutumia mbinu za kisasa zaidi za kilimo.
Amesisitiza kuwa badala ya kutegemea ardhi pekee, wananchi wanaweza kulima kwa kutumia mifuko na ndoo, maarufu kama “plastic gardening”huku akieleza kuwa mbinu hii inasaidia kuboresha afya za familia kwa upatikanaji wa mbogamboga safi, pamoja na kuongeza kipato kwa urahisi.
Picha ya Mkurugenzi wa Taasisi ya (EDO) Bi. Josephine Said Picha na Kuruthum MkataSauti ya Mkurugenzi wa Taasisi ya (EDO) Bi. Josephine Said
Kwa upande wake, mwanafunzi aliyedhamini kutoka Ujerumani Lara Kramer amesema amefurahi kushiriki katika mafunzo hayo pamoja na familia ya EDO huku akibainisha kuwa matumizi ya teknolojia hii rahisi inaweza kusaidia kuongeza kipato bila gharama kubwa, kwani inatumia vifaa vinavyopatikana kirahisi kama mifuko na plastiki hivyo Pia ameongeza kuwa mbinu hiyo inaruhusu upandaji wa mazao mbalimbali ikiwemo bamia na nyanyachungu.
Sauti ya mwanafunzi aliyedhamini kutoka Ujerumani Lara Kramer
Nao baadhi ya wanafunzi wa Taasisi hiyo, akiwemo Aziza Hamis, walisema mafunzo hayo yamewapa uelewa mpya tofauti na walivyozoea ambapo wameahidi kuisambaza elimu hiyo kwa jamii ili kusaidia kuboresha uzalishaji wa mazao na kujikwamua kiuchumi.
Picha ya baadhi ya wanafunzi wa Taasisi ya (EDO) (Picha na Kuruthum Mkata)