Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
2 April 2026, 13:53

Picha ya kituo cha kupoza Umeme Ifakara{Picha na Kuruthum Mkata}
” Uwepo wa kituo hicho umeondoa kwa kiasi kikubwa tatizo la kukatika kwa umeme katika maeneo ya Mng’eta na Mchombe, hivyo REA kwa juhudi zake za kusambaza umeme vijijini na kuomba iongeze kasi katika maeneo mengine”-Meneja Mkuu wa TANESCO Mkoa wa Morogoro Kusini
Na Kuruthum Mkata
Kituo cha kupoza umeme Ifakara kina ziada ya megawati 11 ambazo bado hazijatumika licha ya kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 18
Hayo yameelezwa na Meneja wa Miradi ya kusambaza Umeme kutoka REA Mhandisi Deogratius Nagu wakati wa ziara ya Jukwaa la Wahariri Nchini walipotembelea kituo hicho kilichopo kata ya kibaoni halmashauri ya mji wa ifakara wilayani kilombero leo machi, 31 Ambapo amesema uwekezaji huu umeongeza upatikanaji wa umeme katika wilaya za Malinyi, Kilombero na Ulanga.

Meneja wa Miradi ya kusambaza Umeme kutoka REA Mhandisi Deogratius Nagu{Picha na Kuruthum Mkata}
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi bilioni 25 zilizowezesha ujenzi wa kituo hicho huku Akisema kuwa mradi huo umewanufaisha wananchi huku ukifungua fursa mpya za kiuchumi ikiwemo uanzishaji wa viwanda

Picha ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya(Picha na Kuruthum Mkata)
Naye Meneja wa TANESCO Mkoa wa Morogoro Kusini Mhandisi Masingija Lugata amesema uwepo wa kituo hicho umeondoa kwa kiasi kikubwa tatizo la kukatika kwa umeme katika maeneo ya Mng’eta na Mchombe, hivyo ameishukuru REA kwa juhudi zake za kusambaza umeme vijijini na kuomba iongeze kasi katika maeneo mengine
Aidha, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)Deogratius Balile ameipongeza REA kwa uwekezaji huo, akisema umechochea ukuaji wa fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kuanzishwa kwa viwanda.

Picha ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF)Deogratius Balile (Picha na Kuruthum Mkata)