Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
29 March 2026, 09:17

Hata hivyo, baadhi ya wanawake wamesema bado wameshindwa kunufaika na mikopo hiyo kutokana na kupata usumbufu,ukosefu wa uelewa na wengine hushindwa kufikia vigezo vinavyohitajika
Na Katalina Liombechi
Wanawake Katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wametakiwa kuendelea kuchangamkia fursa za uwezeshwaji kiuchumi kupitia mikopo inayotolewa na serikali kupitia programu mbalimbali, ili kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao pamoja na familia zao.
Wito huo umetolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Bi Renida Magungu, alipokuwa akizungumza na Pambazuko FM.
Hata hivyo, baadhi ya wanawake wamesema bado wameshindwa kunufaika na mikopo hiyo kutokana na kuona usumbufu,ukosefu wa uelewa wa kutosha kuhusu taratibu na masharti ya kupata mikopo hiyo na wengine hushindwa kufikia vigezo vinavyohitajika.

Afisa Maendeleo amesema kuwa wanawake wana nafasi kubwa ya kunufaika na mikopo, ikiwemo ile ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri pamoja na mikopo kupitia Benki (WBN), ambayo imelenga kuwainua kiuchumi wanawake na jamii kwa ujumla.
Aidha amesisitiza umuhimu wa wanawake kujitokeza kwa wingi, kushiriki katika vikundi, na kufuatilia kwa karibu taarifa zinazotolewa na mamlaka husika ili waweze kunufaika kikamilifu na fursa zilizopo.

Amebainisha kuwa serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha mikopo hiyo inawafikia walengwa kwa kugawa fursa hizo kwa usawa, ili kila mwananchi mwenye sifa aweze kunufaika na programu hizo za uwezeshaji kiuchumi.