Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
27 March 2026, 20:57

Miradi hii inatarajiwa kupitiwa na mwenge wa uhuru ikilenga kuboresha huduma za kijamii na miundombinu kwa wananchi wa eneo hilo
Na Kuruthumu Mkata
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya ameongoza Kamati ya Usalama ya Wilaya leo katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 ndani ya Halmashauri ya Mji wa Ifakara.
Ziara hiyo imelenga kujiridhisha na hali ya utekelezaji wa miradi pamoja na maandalizi yake kabla ya tukio hilo muhimu kitaifa.
Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa nishati mbadala uliopo Kata ya Lumemo uliogharimu shilingi milioni 150, pamoja na mradi wa barabara ya Bomani kwa kiwango cha lami uliotumia zaidi ya shilingi milioni 499.
Miradi hii imelenga kuboresha huduma za kijamii na miundombinu kwa wananchi wa eneo hilo.
Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Hoteli ya Homeland katika Kata ya Mbasa, zahanati ya Kijiji cha Sululu, mradi wa maji uliopo Kijiji cha Mpanga, Kata ya Kisawasawa pamoja na mradi wa ushonaji wa vijana wa kike uliopo kata ya mwaya.
Aidha DC Kyobya amesisitiza umuhimu wa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati na kwa viwango vinavyokidhi ubora unaotarajiwa.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wameelezea matarajio yao kupitia miradi hiyo itakapokamilika kwamba itawanufaisha kiuchumi,kijamii na kiafya.
ya Mji wa Ifakara Juni 13, 2026, ukiwa na kaulimbiu isemayo “Tanzania yetu sote, kwa pamoja tushikamane kuleta maendeleo”