Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
26 March 2026, 16:39

Jitihada hizo zimefanikiwa kwa kuungwa mkono na (AWF) kupitia mradi wa Sustain-Eco wanaoutekeleza kwa kushirikiana na IUCN
Na Hospice lipipa/Kuruthumu Mkata
Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa imendelea kuchukua hatua za kupunguza mwingiliano kati ya binadamu na tembo kwa kutoa elimu ya mbinu salama na rahisi za kuwawezesha kuishi pamoja bila madhara.
Jitihada hizo zimefanikiwa kwa kuungwa mkono na Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Afrika (AWF) kupitia mradi wa Sustain-Eco, unaotekelezwa kwa kushirikiana na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (IUCN) na kufadhiliwa na Serikali ya Sweden, ukiwa na lengo la kurejesha mifumo ikolojia.
Akizungumza leo, Mhifadhi Calvin Rembo kitengo cha hima sheria Machi 26, 2026, kupitia Radio Pambazuko FM katika kipindi cha Taswira, amesema kuwa wameielimisha jamii mbinu rahisi za kuzuia tembo kuingia katika maeneo yao na kusababisha uharibifu.