Pambazuko FM Radio

Udzungwa yaimarisha uhifadhi kwa jamii

25 March 2026, 11:20

Picha za wahifadhi kutoka hifadhi ya Udzungwa wakizungumza kupitia Pambazuko FM(Picha na Kuruthumu Mkata)

Kupitia Mradi wa Sustain-Eco, unaotekelezwa kwa ushirikiano wa AWF na IUCN chini ya ufadhili wa serikali ya Sweden, ulitoa zaidi ya shilingi milioni 25 mwezi Oktoba 2025 kusaidia juhudi hizo.

Na Hospice Lipipa/Kuruthumu Mkata

Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa imefanikiwa kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa uhifadhi, udhibiti wa mioto na kukabiliana na wanyamapori waharibifu, kupitia mradi wa mwaka mmoja kwa kushirikiana na Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Afrika (AWF).

Wakizungumza leo march 25,2026 Afisa uhifadhi daraja la pili Calvin Frank Rembo Kitengo cha Hima sheria na ulinzi mkakati pamoja naye Afisa mhifadhi mwandamizi Ahmed Nassor Kitengo cha Utalii kupitia Redio Pambazuko FM Katika kipindi cha Taswira Mradi huo umetekelezwa katika vijiji vya Mwaya,Mang’ula A na Sanje mradi huo umewezesha matumizi ya mbinu shirikishi na endelevu katika kulinda hifadhi na kudhibiti mioto kwa ufanisi na kuzuia muingiliano wa binadamu na tembo na kurejesha mifumo ikolojia.

Kupitia Mradi wa Sustain-Eco, unaotekelezwa kwa ushirikiano wa AWF na IUCN chini ya ufadhili wa Serikali ya Sweden, ulitoa zaidi ya shilingi milioni 25 mwezi Oktoba 2025 kusaidia juhudi hizo.

Karibu kusikiliza kipindi kuhusu udhibiti wa mioto na utalii