Pambazuko FM Radio

Urithishaji maarifa ya asili kusaidia uhifadhi

20 March 2026, 8:03 pm

Picha ya Esther Mtweve afisa maendeleo Ifakara(Picha na Katalina Liombechi)

Afisa maendeleo ya jamii amesisitiza umuhimu wa kuendeleza urithishaji wa maarifa hayo kwa vijana ili yasipotee kutokana na mabadiliko ya maisha ya kisasa

Na Katalina Liombechi

Katika juhudi za kuimarisha uhifadhi wa mazingira na wanyamapori, wataalamu na wanajamii wameendelea kusisitiza mchango mkubwa wa maarifa ya asili yaliyorithishwa kutoka kizazi hadi kizazi.

Hili limebainishwa na Esther Mtweve afisa maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wakati akizungumza leo hii March 20,2026 katika kipindi cha Uhifadhi na Jamii kinachorushwa kupitia Pambazuko FM Radio.

Ameeleza kuwa maarifa ya asili yana nafasi ya kipekee katika kulinda rasilimali za mazingira kwani hujengwa juu ya uzoefu wa muda mrefu wa jamii zinazoishi karibu na mazingira hayo.

Mtweve amesisitiza kuwa mila, desturi na imani za jadi zimekuwa nguzo muhimu katika kudhibiti matumizi ya rasilimali kama misitu, maji na wanyamapori bila kuharibu mfumo wa ikolojia.

Picha ya Easther Mtweve(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Esther Mtweve

Katika kipindi hicho, mwananchi Moses Makereketa alijiunga kwa njia ya simu na kushiriki uzoefu wake kuhusu namna jamii yake ilivyorithi mbinu za asili za kulinda mazingira akieleza kuwa tangu utotoni alifundishwa kuheshimu maeneo ya misitu na vyanzo vya maji, ambavyo vilichukuliwa kuwa maeneo matakatifu yasiyopaswa kuharibiwa.

Sauti ya Moses Makereketa