Pambazuko FM Radio

Wagonjwa wa figo 40 huonwa kwa wiki Ifakara

12 March 2026, 7:24 pm

Picha ya Watumishi Hospitali ya St.Francis(Picha na Kuruthumu Mkata)

Ndani ya siku mbili za wiki Hospitali ya St.Francis huona wagonjwa 30-40 kwa wiki huku wengi wao wakiwa na changamoto ya kifedha kushindwa kugharamia matibabu ya ugonjwa huo

Na Kuruthumu Mkata

Takribani wagonjwa 15 hadi 20 wa figo hupatiwa matibabu kila siku katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Fransisko Ifakara.

Hayo yameelezwa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya figo Katika hospitali hiyo  Dkt. Witness Lubomba wakati wa maadhimisho ya siku ya figo duniani ambayo yamefanyika leo machi,12,2026 katika viwanja vya hospitali hiyo akieleza kuwa mbali na wagonjwa hao wa kila siku, hospitali pia hupokea kati ya wagonjwa 30 hadi 40 wa figo kwa wiki, huku wengi wao wakiwa na changamoto ya kifedha kugharamia matibabu ya ugonjwa huo.

1 Sauti ya Dkt.Witness Libomba

Dkt. Witness ameongeza kuwa magonjwa kama presha na kisukari ni miongoni mwa visababishi vikuu vya matatizo ya figo na kueleza kuwa wagonjwa wengi hufika hospitalini wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa, hali inayopelekea kupata ugumu kwenye matibabu kutokana na gharama kuwa kubwa zaidi.

2 Sauti ya Dkt Witness Lubomba

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Solanus Fussy amesema maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani ni fursa muhimu ya kuikumbusha jamii umuhimu wa kutunza afya ya figo huku akitoa wito kwa jamii kutumia huduma za upimaji wa mara kwa mara zinazotolewa hospitalini hapo.

Picha ya Solanus Fussy Mkurugenzi Hospitali ya St.Francis(Picha na Kuruthumu Mkata)
3 Sauti ya Solanus Fussy mkurugenzi St.Francis

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupima afya zao katika hafla hiyo wameishukuru hospitali kwa huduma hiyo, wakisema elimu na vipimo vinawasaidia kutambua hali ya afya zao mapema na kuwashauri wananchi wenzao kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo mapema.

4 Sauti ya Wagonjwa/wananchi

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya figo duniani inasema  ”afya ya figo kwa wote,jali watu,linda dunia