Pambazuko FM Radio

Maarifa ya biashara yaongeza mafanikio

11 March 2026, 10:53 pm

Moja ya mashine za mjasiriamali Bahati – Picha na; Bahati Milanzi

Wajasiriamali wa Ifakara wamehimizwa kupata elimu ya biashara, kuweka kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi pamoja na kujenga utamaduni wa kuweka akiba ili kuimarisha biashara zao na kuongeza kipato cha familia.

Na: Isidory Mtunda

Wajasiriamali katika mji wa Ifakara wilayani Kilombero wameelezwa kuwa kukosekana kwa maarifa sahihi ya biashara na usimamizi wa fedha ni miongoni mwa sababu zinazochangia baadhi yao kushindwa kukuza au kuendeleza biashara zao.

Evarista Kessy wa shirika la kazi start fund – picha na: Evarista

Akizungumza kuhusu changamoto hizo, mwakilishi kutoka taasisi ya mikopo Kazi Start Funding Tanzania tawi la Ifakara, Evarista Bonaventure Kessy, amesema wajasiriamali wengi hutumia muda, nguvu na rasilimali nyingi katika biashara bila kupata matokeo yanayotarajiwa kutokana na kukosa taarifa na ujuzi wa usimamizi wa biashara.

Sauti ya Evarista Kessy

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Ifakara Town Council, Theresia Moses Chibada, amewashauri wajasiriamali kuzingatia utunzaji wa kumbukumbu za mauzo na matumizi ili kuwasaidia kupima maendeleo ya biashara zao na kufanya maamuzi sahihi ya kifedha.

sauti ya Thedy Moses

Akizungumzia uzoefu wake wa biashara, Bahati Stiven Milanza, mjasiriamali kutoka kata ya Lipangalala anayejishughulisha na uuzaji wa kuku wa kienyeji, soseji, piza na baga, amesema mafanikio aliyoyapata yametokana na nidhamu ya kuweka kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi, hatua inayomsaidia kufuatilia mtaji wake na kuepuka hasara katika biashara.

Bahati Bonaventure Milanzi – picha na; Bahati Milanzi
sauti ya Bahati Milanzi

Naye Restuta Adolfu Malipula, mjasiriamali mdogo anayefanya biashara ya mama lishe katika mazingira yenye changamoto za vitendea kazi, amesema ameweza kuboresha maisha yake kwa kuweka akiba kidogo kidogo benki kupitia mapato ya biashara yake hadi kufanikiwa kujenga nyumba ambayo sasa anaipangisha.

sauti ya Restuta Malipula