Pambazuko FM Radio

Watendaji 61 wapatiwa mafunzo kupinga ukeketaji kinywani

11 March 2026, 8:21 pm

Picha ya Dkt.Nila Jackson Meneja Mradi wa IOM(Picha na Kuruthumu Mkata)

Mafunzo hayo yanatolewa katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji wa Ifakara lengo ni kuwafikia viongozi wa mitaa/vijiji na kata 817

Na Kuruthumu Mkata

Zaidi ya watendaji 61 kutoka kata za Lumemo na Michenga katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara wamefikiwa na mafunzo kupitia Mradi wa Ukeketaji wa Kinywani kwa Watoto wachanga (IOM) unaolenga kutokomeza vitendo vya ukeketaji wa viungo vya kinywani.

Mafunzo hayo yamefanyika Machi 11, 2026 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Ifakara yakiwahusisha watendaji wa kata, madiwani pamoja na watoa huduma wa afya ngazi mbalimbali.

Akizungumza wakati wa semina hiyo Mratibu wa Huduma za Afya ya Kinywa na Meno wa halmashauri hiyo Dkt. Abdallah Malangalila, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo watendaji hao ili waweze kutoa elimu sahihi kwa jamii na kusimamia upotoshaji uliopo kuhusu vitendo vya ukataji wa udata na kimeo.

Aidha Dkt. Malangalila amewataka Watendaji hao kuhakikisha wanazingatia miongozo ya utoaji rufaa kwa wananchi wanaobainika au kudhaniwa kuwa na changamoto za afya ya kinywa ili waweze kupata huduma stahiki kwa wakati.

Sauti ya Dkt.Abdalah Malangalila

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Michenga khamimu barkadha amesema awali wananchi wengi walikuwa hawaelewi maana ya ukeketaji wakidhani unahusu ukatili kwa wanawake pekee hivyo amesema elimu hiyo imewasaidia kufahamu kuwa pia kuna ukeketaji wa kinywa kwa watoto ambao unaweza kusababisha madhara makubwa kiafya na hata kupelekea kifo.

Sauti ya Diwani wa Michenga

Baadhi ya watendaji walioshiriki mafunzo hayo wamesema wameyapokea kwa uelewa mzuri na wako tayari kuifikisha elimu hiyo kwa jamii.

Picha ya Washiriki wa mafunzo(Picha na Kuruthumu Mkata)
Sauti za wanufaika wa mafunzo