Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
7 March 2026, 11:59 am

Maadhimisho ya siku ya wanawake yanafanyika kwa ajili ya kutafakari mchango wa mwanamke katika jamii na kuhakikisha anajikomboa zaidi
Na Amina Mrisho
Mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto Mila potofu kwa watoto wa kike vimetajwa kuwa bado ni changamoto katika Halmashauri ya mji wa Ifakara.
Hayo yamebainishwa kupitia risala ya wanawake katika maadhimisho ya siku yao ambayo katika Halmashauri hiyo imeadhimishwa March 5 katika kata ya Mwaya Tarafa ya Mang’ula iliyosomwa na bi.Nusura Mlandula.
Mbali na changamoto hiyo,pia amebainisha kuwa kuna changamoto ya ukosefu wa maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya wanawake kufanya shughuli za ujasiriamali.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Ifakara ambaye pia ni Afisa utumishi ndugu Rashid Semngoya amesema kuwa Maadhimisho ya siku ya wanawake yanafanyika kwa ajili ya kutafakari mchango wa mwanamke katika jamii na kuhakikisha anajikomboa zaidi kiuchumi ,kutoa fursa kwa viongozi na jamii katika kuchangamkia fursa mbalimbali ili kujiimarisha kiuchumi.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hufanyika kila mwaka Machi 8, na mwaka huu 2026 yanafanyika chini ya kaulimbiu isemayo: “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi Kufikia Dira 2050.”
Maadhimiasho hayo mwaka huu Katika Mkoa wa Morogoro yanatarajiwa kufanyika Mikese katika viwanja vya Shule ya Msingi Fulwe huku mgeni rasmi anatarijiwa kuwa Mkoa wa Morogoro Mh.Kigoma Malima.