Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
7 March 2026, 10:11 am

Watu wengi hugundulika na magonjwa katika hatua za mwisho kutokana na kutojenga tabia ya kupima afya mapema
Na Katalina Liombechi
Jamii yahimizwa kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa na kuboresha afya zao kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Afisa Afya wa Kata ya Lipangalala Ally Ubwa wakati akizungumza na Pambazuko FM.
Afisa Afya huyo amesema kuwa watu wengi hugundulika na magonjwa katika hatua za mwisho kutokana na kutojenga tabia ya kupima afya mapema.
Ameeleza kuwa magonjwa kama shinikizo la damu, kisukari na magonjwa mengine yasiyoambukiza yanaweza kudhibitiwa iwapo yatagunduliwa mapema.

Baadhi ya Wananchi katika Halamsahuri ya Mji wa Ifakara wamesema wameshuhudia ndugu jamaa na marafiki wakiingia gharama kubwa ya matibabu na wengine kupoteza maisha kutokana na kutofahamu afya zako katika hatua za awali kama wanavyoeleza.