Pambazuko FM Radio

Viwanjasitini yavuka lengo uandikishaji Wanafunzi

20 February 2026, 7:37 pm

Picha ya Edwin Mkonga Mratibu elimu kata ya Viwanjasitini(Picha na Katalina Liombechi)

Uandikishaji wa darasa la awali umefikia asilimia 106, huku darasa la kwanza likifikia asilimia 136 ya lengo

Na Katalina Liombechi

Kata ya Viwanjasitini, Halmashauri ya Mji wa Ifakara, imevuka malengo ya uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza kwa mwaka huu wa masomo.

Mratibu wa Elimu wa kata hiyo, Edwin Mkonga, amesema uandikishaji wa darasa la awali umefikia asilimia 106, huku darasa la kwanza likifikia asilimia 136 ya lengo.

Hata hivyo, ameweka wazi kuwa ongezeko la wanafunzi limeleta changamoto ya upungufu wa walimu, ambapo kwa sasa wanashirikiana na wazazi kupata walimu wa kujitolea wakati wakisubiri ajira rasmi.

Sauti ya Mratibu Elimu

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ifakara, akizungumza Februari 19, 2026 baada ya kikao cha wazazi kilichofanyika shuleni hapo, amesema wazazi wamekubali kushirikiana bega kwa bega na walimu katika kuboresha lishe ya wanafunzi pamoja na kutatua changamoto nyingine zinazoikabili shule, kwa lengo la kuinua kiwango cha taaluma.

Picha ya Esther Nuruva Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Ifakara(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Mwalimu Mkuu

Aidha, wazazi wamekubali kushirikiana na shule katika kuboresha lishe na kutatua changamoto nyingine, kwa lengo la kuimarisha elimu ya watoto wao.

Picha ya Wazazi wakiwa kwenye kikao Shule ya Msingi Ifakara(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Mzazi

Ushirikiano huu kati ya shule na wazazi unachukuliwa kuwa muhimu katika kuhakikisha mazingira ya shule ni salama, yenye kuendeleza maadili mema na maendeleo endelevu ya watoto.