Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
11 February 2026, 8:29 pm

Mkandarasi alipata changamoto ya vifaa kuharibika.
Na Amina Mrisho
Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) wilaya ya Kilombero umeeleza sababu za kuchelewa kusambaza vifusi katika barabara za halmashauri ya mji wa Ifakara.
Akizungumza na Pambazuko FM, Februari 9,2026 Meneja wa TARURA wilaya ya Kilombero,Mhandisi Sadiq Karume, amesema ucheleweshaji huo umetokana na kuharibika kwa baadhi ya vifaa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.

Aidha, amewataka wananchi kutunza miundombinu ya barabara.
Ikumbukwe kuwa mapema mwezi Januari, Pambazuko FM ilitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Kiyongwile A ilijionea na wananchi walieleza changamoto wanazokumbana nazo kutokana na vifusi kuchelewa kusambazwa.