Pambazuko FM Radio

Mitazamo potofu kikwazo wananchi kutibiwa mabusha Ifakara

10 February 2026, 8:38 pm

Picha Hamis Ngayungwa Mratibu magonjwa yasiyopewa kipaumbele Ifakara(Picha na Katalina Liombechi)

“Baadhi ya wagonjwa wanaofika hospitalini wanadai wapo wengine mitaani lakini hawajapata ujasiri wa kujitokeza kutokana na mitazamo potofu”

Na Katalina Liombechi

Mratibu wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi  Kipaumbele katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Hamis Ngayungwa, ameitaka jamii kuacha imani potofu kuhusu ugonjwa wa mabusha na badala yake kufika hospitali kupata matibabu yanayotolewa bure.

Akizungumza na Pambazuko FM kuhusu kampeni ya upasuaji wa mabusha inayoendelea katika Kituo cha Afya Kibaoni tangu Januari 26, 2026, Ngayungwa amesema mwitikio bado si wa kuridhisha licha ya baadhi ya wananchi kujitokeza.

Sauti ya Hamis Ngayungwa

Kwa upande wao, baadhi ya wakazi wa Viwanjasitini wamewahimiza wagonjwa wa mabusha kujitokeza mapema kwa matibabu na kuachana na dhana zisizo na msingi.

Picha ya Kamguna Mkazi wa Viwanjasitini(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Kamguna na Kisweka

Aidha Ngayungwa ameuelezea ugonjwa wa mabusha na chanzo chake.

Sauti ya Hamis Ngayungwa