Pambazuko FM Radio

Nyuki wasiouma fursa nyingine ya Kipato mbadala Kilombero

7 February 2026, 9:26 am

Picha ya wanufaika wa Mafunzo ya ufugaji wa nyuki wasiouma(Picha kwa hisani ya MACCO)

Tumeamua kutoa elimu ya ufugaji nyuki wasiouma baada ya kuona asali ya nyuki hawa ina gharama kubwa kuliko nyuki wa kawaida

Na Katalina Liombechi

Katika jitihada za kupunguza utegemezi wa rasilimali za asili na kuongeza kipato cha jamii, Shirika la Mazingira Alliance for Community and Conservation (MACCO) lenye makao yake Mang’ula, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, limeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za uhifadhi wa mazingira kwa njia endelevu.

Februari 6,2026 shirika hilo limeendesha mafunzo ya ufugaji wa nyuki wasiouma kwa wafugaji 30 kutoka vijiji sita vya Mang’ula A, Mang’ula B, Magombera, Kisawasawa Tundu na Kanyenja Mafunzo ambayo yamehusisha nadharia na vitendo kuhusu utundikaji wa mizinga, utunzaji wa nyuki na mbinu sahihi za uvunaji wa asali.

Akizungumza kuhusu mafunzo hayo, Mratibu wa Miradi wa MACCO, Bi. Felista Mwalongo, amesema kuwa ufugaji wa nyuki wasiouma ni shughuli rafiki kwa mazingira na yenye manufaa makubwa kiuchumi, na kuongeza kuwa shirika litaendelea kushirikiana na jamii kuboresha maisha ya wananchi na kulinda rasilimali za asili.

Amesema baada ya mafunzo hayo washiriki watapatiwa mizinga maalum ili kuanza ufugaji kama chanzo cha kipato na njia ya kuchangia uhifadhi wa mazingira.

Picha ya Felista Mwalongo akitoa elimu ya ufugaji nyuki(Picha kwa hisani ya MACCO)
Sauti ya Felista Mwalongo

Kwa mujimu wa Mtaalam wa nyuki Afisa Ufugaji nyuki Katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara amesema asali ya nyuki wasiouma inaaminika kuwa nzuri na yuki hao huzalisha asali kwa wingi zaidi ukilinganisha na nyuki wengine.

Afisa Ufugaji Nyuki Ifakara