Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
23 October 2025, 7:03 pm

Kwa kipindi kirefu wakulima katika bonde la kilombero wamekuwa wakiuza mpunga badala ya kuuza mchele kitu ambacho haishauriwi kwani kufanya hivyo kunapunguza thamani ya zao hilo
Na Kuruthumu Mkata
Serikali kupitia Idara ya Kilimo Halmashauri ya Mji wa Ifakara imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuongeza thamani la zao la mpunga ili kuhakikisha wakulima wanapata tija kupitia zao hilo.
Licha ya hatua ambazo zinachukuliwa baadhi ya wakulima wamekuwa wakiuza mpunga badala ya mchele ambao unakuwa na thamani na kipato kikubwa kama wanavyoeleza.
Hata hivyo mmoja wa wakulima Ifakara amesema yeye huwa anauza mchele huku akiwataka wakulima wengine kubadili mtazamo,kuacha kuuza mpunga kwani kufanya hivyo kuna hasara kubwa.
Mmoja wa Wafanyabiashara wa Mchele Said Nakapala amesema kuna faida kubwa kuuza mchele huku akitoa wito kwa wakulima kuuza Mchele badala ya Mpunga.
Afisa Kilimo na pembejeo Halmashauri ya Mji wa Ifakara Emmanuel Kadilo akizungumza na Pambazuko FM Ofisini kwake amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima kuzalisha kwa tija na kuongeza thamani ya zao la mpunga kwa kusindika na kupata bidhaa zingine itakayosaidia kumwongezea kipato.
