Pambazuko FM Radio

Dkt. Nchimbi: Wakulima watarajie kilimo chenye tija

18 October 2025, 8:23 pm

Picha ya baadhi ya wananchi kwenye Mkutano wa Dkt.Nchimbi Kilombero(Picha na Kuruthumu Mkata)

Mkutano huo katika kata ya Mwaya ulihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa CCM wa kitaifa na mkoa, ambao walisisitiza mshikamano na amani katika kipindi chote cha kampeni na hata baada ya uchaguzi

Na Katalina Liombechi

Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo amefanya ziara yenye hamasa kubwa katika viwanja vya shule ya msingi Mwaya, Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Katika mkutano huo wa kampeni uliovuta maelfu ya wakazi wa Kilombero na maeneo jirani, Dkt. Nchimbi aliwaomba wananchi kumuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa ubunge na udiwani wa chama hicho.

Akihutubia wananchi, Dkt. Nchimbi alisisitiza dhamira ya serikali ya CCM kuendelea kuboresha maisha ya wananchi kupitia sekta muhimu kama elimu, afya, kilimo, na miundombinu ya barabara, ikiwa Dkt. Samia ataendelea kupewa ridhaa ya kuiongoza nchi.

Picha ya Mgombea mwenza Urais CCM Dkt.Nchimbi(Picha na Kuruthumu Mkata)
Sauti ya Dkt.Nchimbi

Akizungumza Mgombea Ubunge jimbo la Kilombero Mh.Abubakar amemwwleza Dkt.Nchimbi kuwa wananchi wa Kilombero wana uhitaji wa Barabara za mitaa,wana changamoto ya Migogoro ya tembo na Binadamu huku akishukuru kwa utekelezaji wa miradi mingi katika maeneo mnalimbali ambayo kabla ya uongozi wa Dkt.Samia ilikuwa ngumu kutekelezeka.

Picha ya Abubakar Asenga Mgombea ubunge Kilombero(Picha na Kuruthumu Mkata)

Dkt.Nchimbi amewahakikishia wakazi wa Kilombero kuwa miradi mikubwa ya maendeleo itaendelea kupewa kipaumbele, hasa maeneo ya vijijini, ili kuleta usawa na ustawi wa Taifa zima.

Mwenyekiti wa CCM Kilombero Ndug.Mohamed Msuya amesema Chama hicho kimejenga imani kubwa kwa wananchi wa Kilombero huku akimuhakikishia ushindi wa kishindo kwa wahombea wote wa CCM.