Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
17 October 2025, 7:55 pm

“Naomba mnichague nitahakikisha watu wote wanapata mikopo bila kuonewa “
Na Katalina Liombechi
Mgombea Udiwani Kata ya Viwanjasitini kupitia Chama cha Mapinduzi Flora Kwangu leo akizindua Kampeni zake amesema miongoni mwa mambo atakayoshughulikia ni pamoja na changamoto ya Miundombinu ya barabara na kuwa sauti kwa wanawake wanaozalilishwa na mikopo kichefuchefu.
Kupitia hadhara hiyo katika Mkutano alioufanya Mtaa wa Minarani akiomba ridhaa ya kuchaguliwa kwa nafasi hiyo amesema hayo yanakwenda kufanyika kutokana na Ilani ya chama hicho ikigusa pia masuala ya elimu,Afya na uchumi wa watu.
