Pambazuko FM Radio

AGRICOM mshindi maonesho ya Nane Nane

14 August 2025, 4:05 pm

Picha kuonyesha zana mbali mbali za kilimo katika Banda la AGRICOM- Picha na Isidory Mtunda

Kampuni ya AGRICOM Africa Limited imeibuka mshindi wa pili katika Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane 2025 kanda tya Mashariki, yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa makampuni yanayojishughulisha na uuzaji wa zana za kilimo, kutokana na mchango wake mkubwa katika kuhamasisha matumizi ya zana bora za kisasa za kilimo.

Na: Isidory Mtunda

Kampuni ya AGRICOM Africa Limited, inayouza zana za kisasa za kilimo mkoani Morogoro, imeibuka mshindi wa pili katika Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane mwaka huu, na kutunukiwa kombe maalum kutokana na mchango wake mkubwa kwa wakulima.

Picha ya Madaraka Mdesa akiwa amebeba Kombe la mshindi II – Picha na Isidory Mtunda

Akizungumza na Pambazuko FM mara baada ya kukabidhiwa kombe hilo, Afisa Mauzo wa kampuni hiyo, bwana, Madaraka Mdesa, amesema ushindi huo umetokana na uaminifu katika kuuza zana bora za kilimo, ambapo hadi kufikia kilele cha maonesho hayo wamefanikiwa kuuza zaidi ya matrekta matatu

Sauti afisa mauzo AGRICOM – Madaraka Mdese

Kwa upande wake meneja Tawi la Ifakara, bi, Graceana makungu amesema katika maonesho hayo ya Nane Nane 2025, wamepeleaka zana mbali mbali za kilimo kwaajili ya mkulima, ambazo zinaweza kumsaidia mkulima, kuanzia hatua ya kulima hadi kuvuna, na hivyo kupunguza upotevu wa mzao kwa mkulima, inayosababishwa na zana duni za kilimo.

Picha ya Meneja wa tawi la Ifakara- AGRICOM – Bi. Graceana – Picha na Isidory Mtunda

Sauti ya Meneja wa AGRICOM Ifakara – bi; Graceana Makungu

Naye Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, Mhandisi Romanus Myeye, amesema AGRICOM imesaidia vijana waliopata mikopo ya asilimia 10 kwa kuwapatia zana za kilimo ikiwemo Pawatila.

Picha ya Mhandisi Romanus Myeye – Mlimba – Picha na: Isidory Mtunda

sauti ya Mhandisi R. Myeye

Elias Masasili ni mkulima wa halmashauri ya Mlimba alifika kutembelea banda la AGRICOM AFRICA LTD, na hapa anasema kuwa katika banda hilo, amevutiwa na trekta, anaamini kuwa akilipata litarahisisha na kuboresha kilimo chake hivyo ataondokana na jembe la kukokotwa la Ng’ombe – PLAU.

Moja ya Trekta zinazouzwa na Kampuni ya AGRICOM – Picha na Isidory Mtunda

sauti ya bwana Elias Masasila

Maonesho ya Nane Nane 2025 yameendelea kuwa kichocheo muhimu cha kuwakutanisha wakulima, wajasiriamali na wadau wa maendeleo ya kilimo kanda ya ya Mashariki, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema, “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025″