Pambazuko FM Radio

Wanachama wa UKICU Walalamikia Ucheleweshaji wa Malipo ya Mazao Ifakara

30 July 2025, 11:11 am

Wanachama wa UKICU wamelalamikia ucheleweshaji wa malipo ya mazao kwa zaidi ya saa 72, kinyume na utaratibu wa kawaida, katika mkutano mkuu uliofanyika mjini Ifakara – Morogoro.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa UKICU – Picha na Katalina Liombechi

Na; Isidory Mtunda

Wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ulanga KilomberoCooperative UNION – UKICU,  wamelalamikia ucheleweshwaji wa malipo ya mauzo ya mazao yao kwa zaidi ya saa 72 kinyume na utaratibu wa kawaida unaoelekeza malipo kufanyika ndani ya muda huo.

Wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ulanga Kilombero wakifuatilia mkutano Ifakara mjini. picha na; Katalina Liombechi

Malalamiko hayo yalitolewa katika mkutano mkuu wa wanachama wa UKICU uliofanyika katika Ukumbi wa Vijana wa Mtakatifu Yohane Paulo II, Halmashauri ya Mji wa Ifakara, mkoani Morogoro.

sauti ya mwanachama wa UKICU

Akijibu hoja hiyo, Meneja wa UKICU, bwana Anthony Sumangulu Haule, alisema ucheleweshaji huo unachangiwa na sababu mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya mfumo wa malipo kutoka kupitia vyama vya msingi hadi moja kwa moja kupitia chama kikuu. Aliongeza kuwa matatizo ya usajili wa majina tofauti na namba za simu visivyolingana na taarifa za wakulima pia yamekuwa kikwazo.

Meneja wa UKICU Anthony sumangulu Haule

Sauti ya Meneja wa UKICU A.S. Haule

Aidha, wanachama walieleza kuwepo kwa changamoto ya kucheleweshewa malipo ya tozo kwa vyama vya msingi vinavyotumia mfumo wa stakabadhi ghalani. Kwa mujibu wa utaratibu, chama cha msingi hupaswa kulipwa Shilingi 52 kwa kila kilo ya mazao inayohifadhiwa ghalani. Ucheleweshaji huu unasababisha vyama vya msingi kushindwa kujiendesha kwa ufanisi.

picha ya mwanachama akiuliza swali kwa uongozi wa UKICU – Picha na; Isidory Mtunda

sauti za wajumbe wakiuliza kuhusu kero ya Tozo

Akitoa maelekezo kufuatia malalamiko hayo, Kaimu Mrajisi wa Mkoa wa Morogoro, bwana Christus Mushumbusi, alimwagiza Meneja wa UKICU kuhakikisha kuwa suala la malipo ya tozo linapatiwa suluhisho ifikapo Agosti 1, 2025.

Kaimu Mrajisi wa mkoa C. Mshumbuzi

Sauti ya kaimu mraji mkoa C. Mshumbusi