Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
2 July 2025, 8:18 pm

Kilimo shadidi ambacho kinatumia Mbegu kidogo,maji kidogo kinaleta kipato kikubwa na kuinua uchumi wa Mkulima
Na Kuruthumu Mkata
Taasisi inayojihusisha na Utafiti wa mbegu Tanzania TARI Ifakara waendelea kunufaisha jamii kwa kutoa elimu ya matumizi ya bora za kilimo za mpunga na kulima kisasa kwa kutumia teknolojia ya kilimo shadidi.
Hayo yaameelezwa leo Julai 2,2025 na Mtafiti wa mbegu bora za mpunga kutoka Taasisi hiyo Theodor Thomas wakati wa uzinduzi wa Siku ya Mkulima ambayo imefanyika katika Kijiji cha Katurukila kata ya Mkula Halmashauri ya Mji wa Ifakara ambapo pamoja na mambo mengine akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya ameelezea historia ya mradi wa Kilimo hicho chenye tija kinachotumia mbegu kidogo,maji kidogo na mavuno mengi na kwamba inasaidia kupunguza hewa ukaa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstun kyobya Mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema kwa kulima kisasa kutumia teknolojia hiyo ni wazi kuwa vijana watanufaika zaidi kutokana na kilimo shadidi kinajali mazingira na endelevu hivyo kusaidia kukua kiuchumi wakati huo mazingira yanabaki kuwa salama.

Kwa upande wa wananchi wa kijiji cha Katurukila ambao wameonyesha nia ya dhati kulima kilimo hicho wameishukuru TARI kwa elimu waliyopatiwa juu ya kilimo shadidi huku wakitarajia kuondokana na hali ya umasikini na kwamba wataiambukiza elimu hiyo kwa wananchi wenzao.

Mmoja wa wakulima wa Mfano salum ally ambaye pia mwenyekiti wa Kijiji hicho ameelezea kunufaika kupitia kilimo hicho na kwamba amekuwa akijivunia elimu anayoipata kutoka TARI.