Pambazuko FM Radio

Wananchi wakubaliana kujitolea ufunguzi wa barabara

30 June 2025, 10:19 am

Picha ya wananchi wa Kitongoji cha Uwanja wa Ndege wakiwa kwenye mkutano wa hadhara(Picha na Katalina Liombechi)

Maendeleo ya wananchi yanaaza na wao wenyewe kuonyesha utayari na kujitoa na serikali inaunga mkono jitihada zao

Na Katalina Liombechi

Wananchi wa Kitongoji cha Uwanja wa Ndege, kilichopo katika Kata ya Kibaoni ndani ya Halmashauri ya Mji wa Ifakara wamefanya mkutano wa hadhara siku ya ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Jeremiah Machibya kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo.

Katika mkutano huo uliofanyika June 28,2025 agenda kuu ilikuwa ni kujadili mapendekezo ya kuzifungua na kuziendeleza barabara za ndani ya kitongoji hicho kwa lengo la kuziwezesha kusajiliwa rasmi na kutambuliwa na Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Picha ya Jeremiah Machibya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Uwanja wa ndege(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Jeremiah Machibya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Uwanja wa ndege

Wananchi walipokea kwa moyo mapendekezo hayo wakieleza kuwa hatua hiyo itaboresha miundombinu, kuongeza usafiri na kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mbali na ajenda hiyo kuu masuala mengine yaliyopatiwa nafasi katika mkutano huo ni pamoja na changamoto za usafi kwa baadhi ya maeneo ya watu,ulinzi na usalama Wananchi walihimizwa kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi katika kudumisha amani na utulivu ndani ya kitongoji.

Kuhusu suala la lishe Mashuleni ilisisitizwa umuhimu wa lishe bora kwa wanafunzi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuinua kiwango cha ufaulu na afya ya watoto shuleni.

Aidha Wananchi walijadili na kuomba uanzishwaji wa soko la kudumu katika eneo la kitongoji hicho ambapo Mwenyekiti alieleza kuwa tayari kuna eneo linalofaa kwa soko hilo, na jitihada za kulitambua na kulitumia rasmi zinaendelea.

Picha ya Faith Peter Mwananchi wa Uwanja wa ndege(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya wananchi wa Uwanja wa Ndege

Mkutano huo ulihudhuriwa na wakazi mbalimbali wa kitongoji na uliendeshwa kwa mafanikio makubwa, ukionesha mshikamano na mwitikio chanya wa wananchi katika kushiriki maendeleo ya jamii yao huu wito ukitolewa wananchi kuwa na kawaida ya kuhudhuria mikutano kwa lengo la kuijenga Uwanja wa ndege.