Pambazuko FM Radio

Ifakara yahamasisha michezo jumuishi

21 June 2025, 9:35 am

Picha ya Majaliwa Mbugi Afisa utamaduni Ifakara(Picha na Katalina Liombechi)

“Michezo haijabagua nani acheze nani asicheze, ushirikishaji wa watu wenye ulemavu changamoto tunayoipata ni miundombinu sio rafiki”

Na Katalina Liombechi

Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Majaliwa Mbugi amesema kuwa juhudi kubwa zinaendelea kufanyika kuhamasisha ushiriki wa wananchi wote katika michezo, wakiwemo watu wenye ulemavu.

Akizungumza na Radio Pambazuko FM hivi karibuni Afisa huyo amesema licha ya changamoto ya miundombinu isiyokidhi mahitaji ya watu wenye ulemavu, bado wanatamani kuona kila mtu anashiriki kikamilifu kwenye shughuli za michezo na burudani kwa ajili ya afya, mshikamano na kukuza vipaji.

Aidha ametoa wito kwa jamii na wadau mbalimbali kushirikiana na serikali kuboresha mazingira ya miundombinu ya michezo jumuishi kwa wote bila ubaguzi huku akiwataka watu wenye ulemavu wenye vipaji vya michezo wafike katika Ofisi za Utamaduni ili kuona namna ya kukuza vipaji vyao.

Picha ya Majaliwa Mbugi Afisa utamaduni Ifakara(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Majaliwa Mbugi Afisa utamaduni Ifakara