Pambazuko FM Radio

NGOs zatakiwa kufanya kazi kwa kufuata utaratibu

20 June 2025, 8:07 pm

Picha ya wana Jukwaa la NGO’s Kilombero wakiwa kwenye kikao (Picha na Katalina Liombechi)

Uwepo wenu ni chachu kubwa ya maendeleo tunazo NGO’s zisizopungua 48 zingine hazitambuliwi.

Na Katalina Liombechi/Kuruthumu Mkata

Mashirika yasiyo ya kiserikali Wilaya ya Kilombero wamekutana leo katika kikao cha Jukwaa hilo kujadili tathmini ya mchango wao kwa Serikali na jamii, pamoja na kueleza mafanikio na changamoto zinazowakabili.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo Ifakara na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Mgeni rasmi katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na mashirika yasiyo ya kiserikali katika maendeleo ya jamii huku akiyataka mashirika hayo kujitangaza zaidi na kuwa kipaumbele kuzitangaza fursa zilizopo Wilayani Kilombero.

Aidha, ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Jamii kuhakikisha kuwa mashirika yote yanatambuliwa rasmi na kuzingatia taratibu zilizowekwa na Serikali.

Picha ya Mh.Dunstan Kyobya DC Kilombero(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya DC Kyobya

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Benitho Miwandu, ambaye pia ni Mkurugenzi wa shirika la Enlighten Development Organization, EDO amesema kikao hicho ni cha kikanuni na kina lengo la kufanya tathmini ya kazi wanazozifanya ili kuhakikisha zinaboresha maisha ya wananchi.

Picha ya Benitho Miwandu Mwenyekiti wa NGO’s(Picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Benitho Miwandu Mwenyekiti wa NGO’s

Kikao hicho kwa mwaka huu 2025 kimefanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Tathimini ya Mchango wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika maendeleo ya Taifa” ikielezea mchango,mafanikio mbalimbali ikiwemo kutoa huduma za kijamii, huku changamoto kubwa zikitajwa kuwa ni pamoja na upungufu wa rasilimali fedha na urasimu wa baadhi ya taratibu za kiserikali.