Pambazuko FM Radio
Pambazuko FM Radio
20 June 2025, 2:06 pm

Picha ya washiriki wa mjadala wa matokeo ya awali ya utafiti unaofanyika kwenye Bonde la Kilombero(Picha na Elias Maganga)
Shughuli zinazoongezeka za kiuchumi na kijamii katika Bonde la Kilombero zinaweza kuleta madhara makubwa zisipoangaliwa kwa umakini.
Na Elias Maganga
Shughuli zinazoongezeka za kiuchumi na kijamii katika Bonde la Kilombero zinaweza kuleta madhara makubwa zisipoangaliwa kwa umakini wa kutosha.
Tahadhari hiyo imetolewa na Profesa Christine Pallangyo, Mkuu wa Ndaki ya Sayansi za Jamii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Mratibu wa Mradi wa Utafiti wa “Critical Zones Africa, South and East.”
Profesa Pallangyo ameeleza hayo Juni 17, 2025, wakati akitambulisha mradi huo wa utafiti kwa wadau wa Bonde la Kilombero katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Edgar Maranta uliopo Ifakara. Mradi huu unahusisha utafiti katika Bonde la Mto Rufiji, kuanzia Bonde la Kilombero hadi Delta yake.
Profesa Christine amefafanua kuwa madhumuni ya mradi huo, ulioanza mwaka 2023 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2027, ni kutathmini hali na uwezo wa mazingira kuhimili ongezeko la shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Hii inajumuisha upanuzi wa shughuli za makazi, kilimo, na uhifadhi katika maeneo muhimu kiikolojia.
Amesema wameamua kufanya utafiti huu katika Bonde la Kilombero kutokana na eneo hilo kuwa nyeti. Zaidi anaeleza umuhimu wa eneo hilo –

Aidha, Profesa Christine alieleza kuwa lengo la kuwakutanisha wadau katika kikao hicho ni kutafuta suluhisho la pamoja kwa mabadiliko makubwa yaliyopo katika afya ya udongo na ubora wa maji, hasa kutokana na ongezeko la watu na shughuli za kilimo. Pia, alisisitiza umuhimu wa kutoa ushauri wa kisera ili kuona umuhimu wa kuomba mabadiliko.
Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho walieleza wasiwasi wao mkubwa kuhusu afya zao kutokana na matumizi ya viuadudu. Waliomba serikali kutoidhinisha matumizi ya bidhaa zenye athari kwa wananchi bila uchunguzi wa kina.

Mradi huu unachunguza zaidi matokeo ya mgongano wa shughuli za kibinadamu kwenye afya ya mazingira (udongo na maji) na jinsi matokeo hayo yanavyorudi kwa jamii. Utafiti huu unafanywa kupitia vyuo vikuu vitano barani Afrika, ikiwemo:
Kila chuo kitakapokamilisha utafiti wake, watatoa ripoti ya bara la Afrika.
Kwa sasa, utafiti huu upo katika hatua za kukusanya taarifa na kufanya vipimo vya maabara na unatarajiwa kukamilika mwaka 2027.