Pambazuko FM Radio

Diwani aguswa ugumu wa matibabu, akabidhi bima za afya CHF 170

18 June 2025, 7:29 pm

Picha ya Mh.Amina Mgelwa diwani kata ya Lupiro akiwa na baadhi ya wanufaika msaada wa bima(Picha kwa hisani ya Mwashiti Kilamilo)

Wanachama wa CHF hupata huduma haraka na kwa urahisi kwenye vituo vya afya vilivyoingia mkataba na bima hiyo hivyo hupunguza ucheleweshaji wa matibabu unaoweza kusababisha madhara makubwa kiafya

Na Katalina Liombechi

Jumla ya wahitaji 170 katika kata ya Lupiro Wilaya ya Ulanga wamepatiwa kadi za bima ya afya ya CHF na Diwani wa kata hiyo Mh. Amina Seif Mgelwa.

Kadi hizo za bima ya afya ya CHF zimetolewa leo Juni 18, 2025 katika vijiji vya Igota, Nakafulu, Madibira na Lupiro kwa lengo la kurahisisha huduma za afya kwa wahitaji hao hasa wazee.

Akizungumza Mh.Amina amesema kuwa ametoa kadi hizo za bima ya afya kutokana na kuguswa kwani naye aliugua kwa muda mrefu na kwamba ameona adha ya matibabu kwa wagonjwa wasiokuwa na bima za afya.

Picha ya Mh.Amina Mgelwa diwani kata ya Lupiro(Picha kwa hisani ya Mwashiti Kilamilo)
Sauti ya Mh.Amina Mgelwa diwani Kata ya Lupiro

Nilipitia magumu mengi nilipokuwa naugua niliwashuhudia watu wakishindwa kupata matibabu kutokana na kukosa bima.

Baadhi ya wanufaika akiwemo Ally Mbilili kutoka Kijiji cha Lupiro na Imelda Mategana wameshukuru kwa Msaada huo muhimu wakisema kwamba bima hizo zitawasaidia kupata matibabu kwa urahisi kwani mara kadhaa wamekuwa wakipata ugumu wanapougua kutokana na hali duni ya maisha.

Picha ya Imelda Mategana akipeana Mkono na Mh.Amina diwani kata ya Lupiro(Picha kwa hisani ya Mwashiti Kilamilo)

Sauti ya Ally Mbilili kutoka Kijiji cha Lupiro na Imelda Mategana