Pambazuko FM Radio

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru aipongeza Kilombero

18 April 2025, 7:52 pm

Mwenge wa uhuru ulipowasili Ktaika Halmashauri ya Mji wa Ifakara(Picha na Elias Maganga)

“,Miradi yote 14 iliyopitiwa na mwenge imetekelezwa kwa ubora na kwa viwango vinavyotakiwa niwapongeze sana viongozi wa Wilaya ya Kilombero kwa kusimamamia vizuri”-Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Ismail Ally Ussi,

Na Elias Maganga

Mwenge wa uhuru umekagua,kuzindua,kufungua na kuona miradi 7 yenye thamani ya zaidi ya Bil 1 na mil 267 KatikaHalmashauri ya Mji wa Ifakara.

Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri hiyo Aprili 17,2025 viongozi na wadau mbalimbali wameshiriki kikamilifu kwenye shughuli za mapokezi,uzinduzi wa Miradi mbalimbali inayolenga kukuboresha maisha na kuchochea maendeleo ya jamii  kiuchumi.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi Pilly Kitwana Akiupokea mwenge huo kutoka Halmashauri ya Mlimba amesema mwenge huo utakimbizwa umbali wa kilometa 136.1kuanzia eneo la mapkezi katika shule ya msingi kihogosi hadi kwenye makabidhiano Wilayani Kilosa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bi Pilly Kitwana(Picha na Elias Maganga)
Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Pilly Kitwana

Miradi iliyopitiwa na mwenge wa Uhuru ni pamoja ufunguzi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo katika shule ya Msingi Kihogosi kata ya Lumemo ukigharimu Mil 76 na laki 8.

Aidha Miradi mingine ni ujenzi wa  jengo la uzazi katika zahanati ya Michenga wenye thamani  ya Tsh Mil 50,Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kata ya Lipangalala wenye thamani ya Tsh.Mil 80,kuona Mradi wa Vijana Katindiuka Kilimo cha Mbogamboga na Matunda  uliopo kata ya Mbasa Mradi huu unawezeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Enlighten Development (EDO) unagharimu kiasi cha Tsh Mil 12 na laki 4 uliosaidia kupunguza mimba na ndoa za mapema  pamoja na kuleta ustawi wa jamii.

Mradi mwingine ambao umetembelewa ni wa matumizi ya Nishati Mbadala katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ifakara wenye thamani ya Tsh.Mil 5 na laki 2 unaolenga kutunza mazingira na kuchochea matumizi ya Nishati endelevu ikiwa ni miongoni mwa mikakati ya Taifa la Tanzania.

Mwenge wa uhuru pia umezindua mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji Mhelule uliopo kata ya mwaya ukigharimu zaidi ya Mil 542,huku Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mkamba-Ksc kwa kiwango cha Lami ambao umezinduliwa umegharimu kiasi cha Tsh.Mil.499 laki 9 na elfu 61 unaolenga kurahisisha shughuli za Usafirishaji  na kiuchumi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi amepongeza Halmashauri ya Mji wa Ifakara na Wilaya ya Kilombero kwa ujumla kwa maandalizi mazuri na utekelezaji wa miradi yenye tija kwa jamii pamoja naushirikiano wa hali ya juu uliodhihirishwa na Wananchi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi wa katikati aliyeshika maiki(Picha na Elias Maganga)

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero anayeongoza halmashauri za Mji wa Ifakara na Mlimba amesema Mwenge huo pia umetembelea miradi 7 katika Halmashauri ya Mlimba yenye thamani ya Tsh.Bil 2.6

Picha Mkuu Wa Wilaya ya Kilombero Wakili Duntun Kyobya wa Kwanza kushoto

Mwenge wa Uhuru unaendelea na mbio zake katika Wilaya ya Kilosa ambapo itafanya shughuli kama hizo lengo ni kudumisha amani mshikamano na uwajibikaji unaojali ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu 2025 mbio hizo zimebebwa na kauli mbiu isemayo: “Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu 2025 kwa amani na utulivu”