

28 March 2025, 7:06 pm
Wajumbe wa mkutano mkuu chama cha walimu CWT Kilombero – Picha na; Isidory Mtunda
Na; Isidory Mtunda
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Wakili Dunstan Kyobya, ametoa wito kwa viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani humo kuhakikisha wanatatua kero za walimu, kuimarisha umoja miongoni mwao, na kuboresha mahusiano kati ya CWT, wakurugenzi, na maafisa elimu. Kyobya alitoa maagizo hayo Machi 26, 2025, wakati akifungua mkutano mkuu wa CWT wilaya ya Kilombero uliofanyika katika ukumbi wa Edgar Marantha, mjini Ifakara.
katikakati ni DC Kilombero Dunstan Kyobya – Picha na Isidory Mtunda
sauti ya mkuu wa wilaya ya Kilombero
Katika mkutano huo, Mwalimu Jane Ntindya, mjumbe wa kamati ya utendaji taifa, aliahidi kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya katika kutekeleza maagizo yaliyotolewa ili kuboresha maslahi na mazingira ya kazi ya walimu.
sauti ya Mwalimu Jane Ntindya
Zoezi la uchaguzi wa viongozi wapya wa CWT wilaya ya Kilombero lilifanyika, ambapo nafasi mbalimbali zilijazwa. Kwa upande wa uongozi wa walimu kitengo cha KE, nafasi ya Mtunza Hazina ilichukuliwa na Mwalimu Anna Mmary kutoka Shule ya Msingi Miembeni, Halmashauri ya Mji Ifakara, huku nafasi ya Mwenyekiti kitengo KE ikichukuliwa na Mwalimu Ruth John Kaaya wa Shule ya Msingi Kilama A, Halmashauri ya Mji wa Ifakara.
Picha ya Mwalimu Ruth Kaaya akijinadi kuomba ridhaa ya wapiga kura – Picha n Isidory Munda
Katika uongozi wa CWT kwa ujumla, nafasi ya Mtunza Hazina ilichukuliwa na Mwalimu Ally Mrisho Rashid kutoka Shule ya Msingi Kamwene, Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, na nafasi ya Mwenyekiti ilichukuliwa na Mwalimu Daniel Philipo Nyali wa Shule ya Msingi Lipangalala, Halmashauri ya Mji wa Ifakara.
Picha na; Isidory Mtunda
Katika kuhitimisha mkutano huo, Mwenyekiti mteule, Mwalimu Daniel Philipo Nyali, aliwashukuru wajumbe kwa imani yao na kuahidi kusimamia maslahi na haki za walimu wa Wilaya ya Kilombero kwa bidii na uadilifu.
sauti ya mwenyekiti mteule – Daniel Nyali