Pambazuko FM Radio

Mlimba kuongeza uzalishaji zao la Kakao-Kilombero

20 November 2024, 5:10 pm

Na Katalina Liombechi

Tumeona zao hili lina mchango mkubwa wa kiuchumi kwa pato la Halmashauri pia limeleta mabadiliko chanya kwa wakulima hivyo kusaidia Usalama wa chakula kwa ngazi ya kaya na Taifa kwa ujumla.

Kufuatia tija ya Kiuchumi kupitia zao la Kakao Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba inatarajia kuzalisha Jumla ya Miche laki 2 na Elfu 10 ya zao hilo na kugawa bure kwa Wakulima wa Kata Tisa ili kuongeza pato kwa wakulima na Halmashauri kwa ujumla.

Mkuu wa Idara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Katika Halamshauri hiyo Mhandisi Romanus Myeye ameyasema hayo wakati akizungumza na Pambazuko FM Ofisini kwake ambapo pamoja na mambo mengine amesema zao hilo ambalo ni moja kati ya Mazao ya Kimkakati katika Halmashauri hiyo limeonyesha kuwa na mchango mkubwa kwa Pato la Halmashauri na kuleta Mabadiliko chanya ya wakulima.

Sauti ya Mkuu wa Idara ya Kilimo Halmashauri ya Mlimba Mhandisi Romanus Myeye

Mmoja wa Wananchi wa Kata ya Igima ameelezea kuhamasika na kulima Kokoa ili aweze kupata kipato kikubwa na endelevu kupitia zao la Kokoa.

Mwananchi wa Igima Theresia Mwalami(picha na Katalina Liombechi)
Sauti ya Mwananchi wa Igima Theresia Mwalami