Six rivers Africa yawakumbuka watu 114 wenye uhitaji kwa kuwapatia kadi za bima za Afya za matibabu- katindiuka
16 October 2024, 4:08 pm
”Tunawashukuru sana Six River Africa kwa kutupatia msaada wa kadi za bima ya afya bure huu ni msaada kwetu ni mkubwa unapozungumzia uhai wa binadamu kwanza uwe na afya njema hawa ndugu zetu wameona mbali sana tunawashukuru”-wanufaika
Na Elias Maganga
Jumla ya watu 114 katika kaya 19 kata yakatindiukaKATIKA Halmashauri ya Mji wa Ifakara wamepatiwa kadi za bima za afya CHF iliyoboreshwa na shirika la six Rivers Africa
Awali akitoa maelezo ya bima hiyo,zilizotolewa oct 15 mwaka huu Elia matangila ni Afisa mwandikishaji wa bimaya CHF iliyoboreshwaamesema inaanza kufanyakazi baaada ya siku saba kupita tangu kupatiwa kwa bima hiyo na lazima mgonjwa aanzie a zahanati na endapo atapatiwa rufaa aa bima hiyo itaendelea kutumika
Elia matangila ni Afisa mwandikishaji wa bima ya CHF iliyoboreshwa{Picha na Elias Maganga]
Sauti ya Elia matangila ni Afisa mwandikishaji wa bima ya CHF iliyoboreshwa
Naye afisa maendeleo ya Jamii kata ya Katindiuka Milka Pondo amesema kaya 19 zilizochaguliwa ambazo hazifadhiliwi na mradi wowowte lakini zinaonekana zina uhitaji
Sauti ya fisa maendeleo ya Jamii kata ya Katindiuka Milka Pondo
Akizungumza wakati akikabidhi kadi hizo kwa wanufaika Diwani wa kata ya Katindiuka Tatu wakati Njayaga amelishukuru shirika la six rivers Africa kwa msaada huo na misaaada mbalimbali ambayo wameitoa kwa wakazi wa Katindiuka
Picha ya Diwani wa kata ya Katindiuka Tatu wakati Njayaga akigawa kadi za bima ya afya kwa wanufaika Katindiuka{picha na Elias Maganga]
Baadhi ya wanufaika akiwemo Paschal Mabukula ameshukuru kitendo cha kupewa kadi ya bima ya afya ya CHF bure bila malipo ,kwani kabla ya kupatiwa bima hiyo pindi akipata matatizo ya kiafya humlazimu atafute hela ili akapate matibabu tofauti na sasa hata asipokuwa na hela bima hiyo itamsaidia naamewaomba waomba wadau wengine kuiga mfano wa six rivers Africa
Kwa mujibu wa Afisa mradi wa kuboresha watu na wanyama kuishi pamoja kutoka shirika la six Rivers Africa Irene Masonda amesema katika mpango huo kila kijiji wamechukuwa kaya 19pamoja na wategemezi wao watu sita .
Amesema kaya hizo duni zimepatikana kwa ushirikiano kutka kwa wawezeshaji wao kwa kushirikiana na viongozi waliopo katika maeneo yao.
Zoezi hilo la uandikishaji wa biama za afya linaanza rasmi oct15 katindiuka hadi oct 27 litahitimishwa Kijiji cha Miwangani