Wananchi Kilombero jitokezeni kujiandikisha kupiga kura –Dc Kyobya
11 October 2024, 2:00 pm
”Mwananchi atakayejiandikisha kwenye Daftari atapata fursa ya kupiga kura kuchagua au kuchaguliwa na yule ambaye hatajiandikisha hatoshiriki ucahguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Nov 27 mwaka huu” -Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya
Na Elias Maganga
Mkuuwa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya amewaongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na wananchi kwa ujumla katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura lililoanza rasmi hii leo 11oktoba hadi 20 oktoba mwaka huu.
Akijiandikisha kwenye kitongoji cha bomani kilichopo Kijiji cha Kibaoni katika Halmahsauri ya Mji wa Ifakara Mkuu wa Wialaya Kyobya ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Kilombero kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kwani hiyo itamfanya mwananchi apige kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika nov 27 mwaka huu na kwa wale ambao hawatajiandikisha hawatapiga kura.
DC Kyobya amesema Wilaya ya Kilombero ina vitongoji 458 huku ifakara pekee kukiwa na vitongoji 214 na Halmashauri ya Mlimba ina vitongoji 244 hivyo kila mwananchi katika kitongoji chake mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea ajitokeze kushiriki zoezi hilo muhimu la kujiandikisha
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bi Zahra Michuzi amesema mwananchi atakapojiandikisha kwenye daftari la ukaazi atapata haki ya kuchagua ama kuchaguliwa kutokana na sifa zilizoainishwa na Tume ya Uchaguzi,lakini kujiandikisha huko si kwasababu tu ya uchaguzi lakini pia kuisaidia serikali kupanga mipango yake ya baadae ya kujua idadi mahususi ya watu katika eneo husika na huduma za kijamii wanazozihitaji.
Kwa upande wao Sophia Mlela mwenyekiti wa Kitongoji cha Bomani na Frencesianus Zakaria Waya Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibaoni wamesema wananchi wamejitokeza na wanaendelea kujitokeza kujiandikisha na kadri siku zinavyoendelea wanaamini watafikia malengo ya uandikishaji.huku wakiwaomba wananchi kujitokeza wasisubiri siku ya mwisho wani siku hiyo watu watakuwa wengi na wengine wanaweza wakakosa kujiandikisha.
Nao baadhi ya wanananchi waliojitokeza kujiandikisha katika kituo cha chekechea kilichopo kitongoji cha Bomani Fidelis severine na Fida Enock Msola wametoa wito kwa wananchi kujitokeza kujiandikisha kwani wao tayari wameshajiandikisha