Pambazuko FM Radio

Ujenzi wa vizimba Ifakara kuhifadhi mazingira shambani

26 August 2024, 8:09 pm

Na Katalina Liombechi

Wataalam wa kilimo wamewataka wakulima kutumia mbinu sahihi za uhifadhi wa taka sumu mashambani ili kuzuia athari katika udongo na bianuwai.

Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Dkt Dunia Mlanzi ameeleza kuwa uhifadhi wa mazingira mashambani ni muhimu katika kuzuia mmomonyoko wa udongo kwa kutumia mbinu za kilimo endelevu kama vile kilimo kuhifadhi taka sumu katika vizimba hali inayosaidia kuzuia sumu kusambaa na kuharibu viumbe hai vingine.