Mbegu bora mazao ya kimkakati kuzalishwa Ifakara
26 August 2024, 7:41 pm
Na Katalina Liombechi
Halmashauri ya Mji wa Ifakara katika Wilaya ya Kilombero imejipanga kuzalisha mbegu bora za mazao ya kimkakati na kugawa kwa wakulima ili kuhakikisha inapata mapato mazuri.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Dkt.Yuda Mgeni amezitaja mbegu hizo kuwa ni pamoja na miche ya makao, chikichi, korosho na marafuu.
Aidha ametaja sifa za mbegu bora kuwa ni ile iliyothibitishwa kitaalamu, inayotumia muda mfupi na inastahimili magonjwa hivyo mbegu ambazo watakuwa wamezalisha vitalu hivyo zitakuwa zimethibitishwa na kwamba kuanzia Septemba mwaka huu zitakuwa tayari kwenye vitalu huku akiwataka wakulima kuwatumia maafisa ugani katika shughuli za kilimo sambamba na kupata utaratibu wa mbegu hizo zitakavyowafikia.