Pambazuko FM Radio

Kipindi: Umuhimu wa kupima afya ya udongo

26 August 2024, 10:41 am

Na Katalina Liombechi

Inaelezwa kuwa kulima kibiashara inategemea maandalizi mazuri ya shamba ili kufahamu afya na aina ya udongo wa shamba hali itakayosaidia kujua aina ya zao unalopaswa kulima na ni aina gani ya viuatilifu vitakavyohitajika.

Elia Shemtoi ni Mkuu wa Idara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kutoka Halmashauri ya Wialaya ya Kilosa ameyasema hayo wakati akizungumza na Pambazuko FM kuhusu maandalizi ya shamba na umuhimu wa kupima afya ya udongo ili kuzalisha kwa tija na kuzuia matumizi ya viuatilifu kiholela hali ambayo inaweza kuharibu asili ya udongo na kupunguza rutuba ya udongo asilia.