Pambazuko FM Radio

Mizinga bora, ufugaji nyuki kisasa-Kipindi

26 August 2024, 10:27 am

Na Katalina Liombechi

Ufugaji wa Nyuki Kisasa umetajwa kuwa miongoni mwa njia bora ya kukabiliana na tembo sambamba na kuongeza kipato hali inayoweza kupunguza utegemezi wa rasilimali mbalimbali kutoka katika maeneo yaliyohifadhiwa.

Kwa mujibu wa Diana Mahimbali Afisa Ufugaji Nyuki kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa amesema kuwa ufugaji wa nyuki kisasa unahusisha kufuga kwa kutumia mizinga bora iliyotengenezwa kwa mbao nzuri zinazodumu kwa muda mrefu na inahakikishia mavuno mazuri na kulijali kundi la nyuki.