NFRA kuanza kununua mpunga kutoka kwa wakulima Kilombero
5 August 2024, 6:52 pm
“Tumewekwa viongozi ngazi mbalimbali ili tuwasaidie wananchi viongozi mnapo jiingiza kwenye biashara hii na kwenda kunyonya Jasho la mkulima hii sio Sawa haufanyi haki uwe ni Diwani,mwenyekiti sijui wa nini kiongozi ngazi yoyote ile kama unakwenda kudhulumu Jasho la mkulima haufanyi haki mkulima anapoteza nguvu zake ili apate kwa jasho lake na dini zote zinafunsisha kuwa mtu atalipwa kutokana na Jasho lake kwahiyo viongozi tukae chini tujitathimini mara 6 sitamtaja hapa nani ni nani lakini Nina taarifa hizo.–Rais samia Suluh Hassan
Na Elias Maganga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dr Samia Suluh Hassan amewaagiza wakuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa Morogoro kusimamia bei halali ya mazaoya mpunga kwa wakulima Mkoa huo.
Dr Samia amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani KIlombero katika uwanja wa ccm Tangani ambapo amewataka viongozi wa wilaya NA Mkoa wa Morogoro kuhakikisha wanasimamia bei halali ya mazao hususani mpunga ili wlanguzi wasiwakandamize wakulima .
Raisi Samia amesema wakulima wanapozalisha mpunga huwa wanatumia gharama kubwa kwani bei ya mpunga ni ndogo ukilinganisha na gharama wanazotumia ,hivyo wanapovuna anatokea mjanja wa kati anapata faida kuliko mzalishaji amesema hii si sawa.
Pia Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wanaojihusisha na bishara ya ununuzi wa zao la mpunga kujitazama mara 6 na kuacha tabia ya kuwadhulumu wakulima kwa kuongeza kipimo kwenye magunia na kuwalipa kidogo ili wao wanufaike.
Amemwagiza Waziri wa Kilimo kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRAKuanza kununua mpunga kwa kilo shilingi 900tofauti na sasa walanguzi wananunua kwa shilingi 570.
Kwa upande wake waziri wa kilimo Mh Hussein Bashe amemuahidi Dr Samia kuwa kama ataridhia mapendekezo aliyopewa na wizara , Serikali itaanza kununu mpunga kutoka kwa wakulima kuanzia mwezi huu august 2024.