STEP waandaa mashindano ‘Sec Cup’ kuendeleza mahusiano tembo, watu Kilombero
25 July 2024, 12:40 pm
Na Katalina Liombechi
Shirika linalojihusisha na Uhifadhi wa Tembo Kusini mwa Tanzania STEP kupitia kwa Mtafiti wa Shirika hilo Kepha Mwaviko limesema wanaendelea kujenga uhusiano kati ya binadamu na tembo kwa kutekeleza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa michezo kama njia ya kuwakutanisha watu na kuhamasisha wanafunzi kufahamu umuhimu wa kumhifadhi mnyama tembo ili nao wakawe mabalozi kwa wazazi wao.
Mwaviko akizungumza mara baada ya mchezo wa fainali wa mashindano ya ‘SEC CUP’ambayo yamefanyika July 22,2024 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mang’ula A amesema Mashindano hayo yalianza July 15 mwaka huu na yalihusisha Shule mbalimbali za Sekondari ikiwa ni pamoja na Nyange,Bokela,Mwanihana,Mang’ula,Kalunga na Asenga Sekondari ambazo zimeshiriki kwa Michezo Mbalimbali.
Katika Mchezo wa Fainali Upande wa Mpira wa Miguu Timu zilizocheza ni Nyange SEC ambayo imeibuka na Ushindi wa Mabao 2-1dhidi ya Mang’ula Sekondari huku ‘Netball’ Timu zilizocheza ni Bokela ambayo imeibuka na Ushindi wa Mabao 38-22 dhidi ya Mshindani wake Mwanihana Sekondari.
Timu zilizoshinda Fainali zimepata zawadi za Kombe na Kiasi cha Fedha Tsh 300,000/= huku Mshindi wa Pili akipata Tsh 200,000/= na Mshindi wa Tatu akipata TSh 100000/=.
Picha ya Kepha Mwaviko Mtafiti STEP(Picha na Katalina Liombechi)
Wakizungumza Baadhi ya Makaptain kutoka Timu ya Mang’ula A Patrick Kumbunja kwa Upande wa Mpira wa Miguu na Maria Utambule kutoka Timu ya Bokela Mchezo wa Netball wameelezea kulishukuru shirika la STEP kuandaa Mashindano hayo huku wakitamani Tembo aendelee kuhifadhiwa.
Sauti za Makaptain Maria Utambule Bokela Sec(Netball)na Patrick Kumbunja Mang’ula Sec(Mpira wa Miguu)
Beatrice Lihaku ni Mwalimu wa Tembo Kutoka Kitengo cha Mahusiano ya Tembo na Watu STEP ameelezea faida za Kumhifadhi Mnyama Tembo na hatua za kuchukua Mtu anapokutana na Tembo.
Aidha Michezo Mingine iliyochezwa Kunogesha Mashindano hayo ni kuvuta Kamba Pamoja na Kukimbiza kuku.
Ikumbukwe kuwa STEP imesajiliwa mwaka 2014 inafanya Kazi ya Ulinzi wa tembo, utafiti na ufuatiliaji, kuimarisha mahusiano baina ya tembo na watu kupitia miradi ya uhifadhi ya jamii,utetezi na elimu.